Rais Dkt.Mwinyi atoa wito kwa wananchi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj DkT.Hussein Ali Mwinyi amesema amani ndiyo nguzo kuu ya mambo mengine yote bila amani huwezi kuzungumza maendeleo.
"Nchi ina amani, wananchi wana umoja, mshikamano na utulivu kuweza kufanya shughuli za ibada bila hofu yoyote na yatupasa kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu aendelee kutudumishia amani yetu;

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Novemba 3, 2023 baada ya kujumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa Masjid Noor Kombeni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, ni wajibu kuilinda na kuitunza amani ya nchi kwa kila mwananchi na si jukumu la Serikali peke yake kwa kuanzia ngazi ya jamii, pamoja na familia kupitia malezi .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news