Rais Dkt.Mwinyi awashukuru UWT, wafunguka

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuthamini kuandaa mkutano uliojumuisha Wanawake kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa yote ya Tanzania Bara.

Dkt.Mwinyi amesema hayo katika mkutano wa kumpongeza kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 04 Novemba 2023.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ampongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kuimarisha umoja, mshikamano na utulivu wa nchi na kuwaletea maendeleo Wazanzibari.

Amesema, katika miaka miwili iliyobaki utekelezaji wa miradi ya maendeleo utakuwa mkubwa zaidi na Zanzibar baada ya miaka 10 itakuwa ya maendeleo makubwa.

Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT wameridhika na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kwa kuvuka malengo ya utekelezaji ndani ya miaka mitatu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa Zanzibar .

Vilevile ameeleza kuwa UWT watamchukulia na kumjazia fomu ya kuomba Urais wa Zanzibar Dk.Mwinyi pia watafanya hivyohivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan mwaka 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news