Rais Dkt.Samia afanya uteuzi NSSF, Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka na GBT

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bi.Mwamini Juma Malemi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Bi. Malemi ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Prof. Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka.Prof. Mgaya ni Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw.James Bakinege Mbalwe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT) kwa kipindi cha pili.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 17, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus ambapo uteuzi huu umeanza Novemba 14, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news