Rais Dkt.Samia ateua wawili TCRA

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 13, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Dkt.Jones A. Killimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Vile vile, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Juma Hassan Reli kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Uteuzi huo unakuja baada ya Novemba 7,2023 Mheshimiwa Rais Dkt.Samia kuivunja Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news