Rais Dkt.Samia atoa maagizo kwa mabaraza ya michezo

ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Mabaraza ya Michezo kuendelea kuratibu na kufuatilia utendaji wa vyama vya michezo na kuhakikisha vinaendeshwa na kujiendesha kwa manufaa ya taifa.

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati chini ya Umri wa miaka 15 (CECAFA U15) kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys), Mohamed Ali Mohamed wakati wa hafla ya kuipongeza, Ikulu Tunguu Zanzibar.

Rais Samia amesema serikali inapoweka mazingira mazuri katika sekta ya michezo hutoa hamasa kwa wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo kwa kuwekeza katika timu za vijana.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya chakula cha mchana aliyoiandaa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.

Timu ya Karume Boys imetwaa Kombe la Mashindano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yaliyofanyika nchini Uganda ambapo tangu miaka ya 1990 Zanzibar haijawahi kushinda katika mashindano hayo.

Vile vile Rais Samia amesema michezo hutoa fursa ya ajira kwa makundi mbalimbali hususan vijana hivyo viongozi hawana budi kuweka mipango endelevu na kuwekeza katika sekta hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita wa Zanzibar katika picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.

Aidha, Rais Samia ameyataka Mashirikisho ya Soka Tanzania bara na Zanzibar kutumia mapato yanayotokana na viingilio vya mechi kufanya ukarabati wa viwanja badala ya kusubiri matengenezo makubwa ambayo yanaongeza gharama maradufu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshika Kombe la Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati chini ya Umri wa miaka 15 (CECAFA U-15) pamoja na Gloves ya Kipa bora wa Mashindano hayo yaliyofanyika nchini Uganda. Mhe. Rais Samia aliwaandalia hafla ya kuwapongeza Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Benchi la Ufundi la timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kutoa msukumo mkubwa katika kukuza sekta ya michezo nchini ikiwemo kurudisha ligi ya Muungano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news