Serikali yanunua mtambo wa kisasa kufundishia wanafunzi Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI)

DAR ES SALAAM-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Uchukuzi imetumia zaidi ya shilingi bilioni 2.74 kununulia mtambo (Crane Simulator ) ya kisasa wa kufundishia kwa ajili ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).

Mwanafunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam akiwa kwenye mtambo (Crane Simulator) wakati akifanya mazoezi ya kuendesha mtambo huo mpya ambao umenunuliwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.74.

Mkuu wa chuo hicho, Dkt.Tumaini Gurumo amesema,mtambo (Crane Simulator) huo utasaidia kufundishia wanafunzi kwa vitendo na kuongeza thamani ya elimu inayotolewa katika chuo hicho pekee hapa nchini.

“Mtambo huu unasiadia kufundishia katika kozi ambazo utendaji kazi wake ni maeneo ya Bandari, Viwandani na Migodini. Zaidi ya Shilingi bilioni mbili nukta tano imetumika kununulia mtambo huu mpaka kufunga hapa chuoni,”amesema Dkt.Tumaini.

Muonekano wa picha wa mtambo (crane simulator ) ambao Serikali kupita Wizara ya Uchukuzi imenunua kwa ajili ya kufundishia Chuo cha Bahari Dar es Salaam, mtambo huo umenunuliwa kwa zaidi ya shilingi 2,744,106,712.35.

Tumaini ailongeza kuwa, mtambo huo utasaidia sana kwenye mafunzo kwa vitendo, kuongeza uzalishaji wa wanataalamu wenye ujuzi wa viwango vya juu kwani mtambo huu unalenga kujengea uwezo wanafunzi utakaosaidia kuongeza tija katika maeneo mbalimbali.

Msimamizi wa mtambo na mkufunzi wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Elinathan Blasius akitoa ufafanuzi wa namna mtambo unavyofanya kazi na namna ambavyo mwalimu anaweza kumtumia kazi mwanafunzi huku akiendelea kufuatilia utendaji kazi wake.

Elinathan Blasius Mtaalamu wa Mtambo huo na Mkufunzi wa Chuo cha Bahari Dar es salaam amesema kuwa mtambo huo wa kisasa ni muhimu kwa wanafunzi kwani utasaidia kupata elimu ya kuendesha mitambo mabalimbali.

"Kwa kila mtambo huu una mada zaidi ya kumi hivyo kila mwanafunzi atapata elimu ambayo itamsaidia kuendesha mitambo mikubwa na midogo,”alisema Elinathan.
Kwa upande wake Mwalimu Leonard Mwesiga amesema kuwa mtambo huo ni muhimu sana kwa chuo hicho kwani unaweza kufundishia wanafunzi zaidi ya masomo sita na mwanafunzi akihitimu katika masomo hayo ataweza kuendesha mitambo ya aina yoyote katika sekta ya Bandari, Viwandani na Migodini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news