SUZA kuzalisha wataalam bora nchini

ZANZIBAR-Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhamed Mussa, amesema, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kitaendelea kutoa taaluma za fani mbalimbali ili kuhakikisha kinazalisha wataalam walio bora nchini.

Ameyasema hayo wakati akizindua Baraza la Nane la Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) katika ukumbi wa Mikutano Skuli ya Utalii Maruhubi.

Amesema, wajumbe wote walioteuliwa ni watendaji wa Serikali hivyo ni matumaini yake wajumbe hao wanaweza kufanya maamuzi mazuri ya kuendelea kufanikisha mipango na mikakati ya chuo hicho.

Amesema, Zanzibar imekua na ufaulu mkubwa kwa wanafunzi wa Sekondari hivyo SUZA inahitaji kuendelea kuwa na mipango ya kuandaa programu mbalimbali ziatakazopelekea wanafunzi hao kuweza kujifunza kupitia chuo hicho.

Pia aliwataka wajumbe hao kutumia tafiti mbalimbali juu ya miradi mikubwa ili kuleta mageuzi yanayoendana na wakati na kuisaidia Serikali kuweza kukuza Uchumi wa Taifa.

Aidha Waziri Lela amewasisitiza Wajumbe hao kuhakikisha wanaendelea kutatua changamoto za kutanua miundombinu ya upatikananji wa fani ili kuhakikisha wataalamu wanaozalishwa Sekondari wanapata fursa ndani ya Chuo hicho.

Hata hivyo, amewataka wajumbe hao kufanya kazi kwa kushirikiana na wajumbe waliopita ili kuhakikisha wanaiendeleza vyema sekta ya Elimu na kuhakikisha SUZA inatoa vipaombele vya ufundi kwa upande wa Zanzibar.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo la Nane, Bi. Hamida Ahmad Muhammed amempongeza Waziri wa Elimu kwa kuharakishaa kuchagua baraza jengine mara baada ya kumaliza muda kwa Baraza la saba ili kuhakikisha chuo hicho kinaendelea kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) Profesa Mohammed Makame Haji amewasisitiza Wajumbe Wapya kutumia utaalamu uliyobora katika utekelezaji wa kazi zao ili kuweza kuisadia Serikali kufikia malengo yake ya Uchumi wa Buluu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news