Wakulima wapewa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vipimo

NJOMBE-Kikosi kazi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara,Wizara ya Kilimo ,Ofisi ya Rais Tamisemi leo Novemba 20,2023 kimefanya ziara na kufanya mazungumzo na Kaimu Afisa Tawala Msaidizi sehemu ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Bwana Lusungu Esau Mdede mkoani Njombe.

Lengo la ziara hiyo kufanya tathimini ya namna bora mazao ya kilimo yanavyoweza kufungashwa kwa kufuata vipimo sahihi.

Aidha, Bwana Mdede amesema ujio wa kikosi kazi hiki ni tumaini na suluhisho kwa wakulima kwani wengi wamekuwa na hamasa ya kupata. elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo kwani itasaidia katika upatikanaji wa faida zaidi na kuepukana na matumizi ya madebe na visado katika mazao ya kilimo hususani nyanya,vitunguu,karoti,tangawizi na viazi mviringo.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Biashara, Dkt.Hanifa Mohammed Yusuph amesisitiza kuwepo na matumizi sahihi ya vipimo katika mazao kilimo ni muhimu ili kuwezesha upatikanaji wa mapato Serikalini na kukuza ustawi wa biashara nchini.

Wakati huo huo wakulima na wafanya biashara mkoani Njombe wamepewa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya vipimo ili kuepuka hasara na pia adhabu mara watakapobainika kukikuka sheria ya vipimo nchini.

Kilosi kazi hiki kimeanza tathimini hii Novemba 13, mwaka huu kikipitia katika masoko ya jiji la Dar es Salaam,Arusha,Manispaa ya Iringa na mkoa wa Njombe kwa lengo la kutathmini ufungashaji wa mazao ya kilimo yasiyofuata vipimo sahihi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news