Tanzania kuwa mwenyeji wa Tuzo za HAPAawards 2024

DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Tuzo za HAPAwards, Bi.Tina Weisinger na Makamu wake Bi. Amberr Washington.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Novemba 10,2023 jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine wamejadili juu ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo hizo msimu wa nane mwaka 2024.

Mhe. Ndumbaro amewahakikishia viongozi hao kuwa, Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji wa tuzo hizo ambazo zitasaidia kuongeza ubora wa kazi za Sanaa zinazozalishwa nchini.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo Pamoja na watendaji wengine wa Baraza la Sanaa la Taifa na Bodi ya Filamu.

HAPAawards ni miongoni mwa tuzo kubwa za heshima zinazotolewa kwa wasanii wanaofanya vizuri nchini Marekani na Afrika ambapo kwa msimu huu wasanii wawili kutoka Tanzania Jacob Stephen (JB) na Saraphina Michael (Phina) walishinda tuzo hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news