Tanzania yarekodi matokeo chanya mapambano dhidi ya VVU

DODOMA-Imeelezwa kuwa, Tanzania imepata matokeo chanya katika Mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI na kwamba idadi ya maambukizi mapya inaendelea kupungua ikilinganishwa na matokeo ya Utafiti wa mwaka 2016/17.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu kukamilika kwa Taarifa za Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Nchini kwa mwaka 2022/2023 tarehe 31 Oktoba, 2023.

Mhe. Jenista amesema lengo la utafiti huo ni kupima matokeo ya juhudi za mapambano dhidi ya UKIMWI ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya VVU na UKIMWI (Tanzania AIDS Impact Survey - THIS) kila baada ya miaka mitano ambapo Uchakataji wa takwimu zilizokusanywa unaendelea.

“Haya ni mafanikio mazuri ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imeyafikia kuelekea kufikia Malengo ya kitaifa ya kufikia SIFURI TATU – yaani Kutokuwa na Maambukizi Mapya, Kutokuwa na Unyanyapaa na Ubaguzi, na Kutokuwa na Vifo Vitokanavyo na UKIMWI. Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya VVU na UKIMWI ya mwaka 2022/23 itazinduliwa rasmi tarehe 1 Disemba, 2023,” Amesema Mhe. Jenista.

Pia ameeleza kwamba utafiti wa aina hiyo hufanyika kupima mwenendo wa VVU na UKIMWI Duniani, kwa kupima kiwango cha maambukizi mapya na Kufubaa kwa VVU katika ngazi ya jamii hivyo kupitia utafiti huo, serikali itapata taarifa kuhusu viashiria na matokeo ya VVU/UKIMWI katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2022/23 ambazo ni takwimu muhimu kuhusu hali ya UKIMWI nchini.

“Utafiti wa mwaka 2022/23 ni wa Tano kufanyika nchini Tanzania, na wa pili wa aina ya Population Based HIV Impact Assessment - PHIA kufanyika katika ngazi ya Jamii na utafiti wa PHIA kwa mara ya kwanza ulifanyika nchini Tanzania mwaka 2016/17,” Ameeleza.

Aidha Mhe. Jenista amebainisha kuwa Utafiti huo umefanywa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Tume ya Kudhibiti UKIMWI Zanzibar (Zanzibar AIDS Commission- ZAC), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) pamoja na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar (Office of Chief Government Statistician - OCGS).

Akiwataja wadau wengine wa maendeleo walioshirikiana na Serikali amefafanua kuwa ni Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Kinga (Centre for Disease Control - CDC) na Chuo Kikuu cha Columbia (International Centre for AIDS Program I-CAP) na Mpango Jumuishi wa kupambana na UKIMWI, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma (Zanzibar Integrated HIV, Hepatitis.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news