Wananchi watakiwa kujitokeza kupima kwa hiari VVU

MOROGORO-Wito umetolewa kwa wananchi kuendelea kujitokeza kupima VVU kwa hiari ili kujua hali zao ili kuendelea kuishi kwa kuzingatia matokeo, kwa wale ambao hawatakutwa na maambukizi ni nafasi kwao kuendelea kuishi ili wasiambukizwe na wale ambao watakutwa na maambukizi wana nafasi kuendelea kuishi kwa kutumia dawa za kufubaza.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa kikao cha pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Kighoma Malima kuhusu kuelekea maandalizi ya siku ya UKIMWI kitaifa, katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ameongeza kusema tafiti zote za miaka mitano zimeonesha wanaume hawajitokezi kupima, na hawajitokezi kuanza kupata dawa, na hivyo kusumbuliwa sana na magonjwa Nyemelezi yanayotokana na virusi vya UKIMWI.

“Virusi vya UKIMWI na UKIMWI upo ni wajibu wa kila Mwananchi kuendelea kuchukua tahadhari,” alibainisha
Aidha kauli mbiu yetu inyosema; JAMII IONGOZE KUTOKOMZEA UKIMWI inatuhamasisha jamii yenyewe ndio iongoze mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI

Akizungumzia kuhusu malezi, ametoa rai kwa wazazi kukaa na familia na kuwaelimisha uwepo wa tatizo hili la UKIMWI.

“Tunajukumu kubwa la kuendelea kutoa malezi bora kwa watoto wetu na kuwajengea misingi ya tabia njema,” alifafanua.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akiongea jambo wakati wakikao cha maandalizi kuelekea siku ya UKIMWI kitaifa.


Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe.Adam Malima amesema, maandalizi kuelekea wiki Maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanaendelea vizuri
“Lengo ni kupeleka ujumbe kwa wananchi, huku tukitupia jicho kwa kundi la vijana na kwa kushiriki kwao itasaidia kupeleka ujumbe kwa vijana wengine ambao hawakupata fursa ya kushiriki,”alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news