Watumishi wa Afya watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu, ufanisi

TANGA-Naibu Katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt Grace Magembe amewataka watumishi wa afya nchini kuwajibika kwa kufanya kazi kwa ufanisi na uwadilifu ili ili kutimiza malengo ya Serikali ya awamu ya sita ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Magembe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bombo (Tanga) ambapo amesema watumishi wanatakiwa wajitume katika kuwahudumia wananchi.

“Wapo baadhi ya watumishi wanaofanya kazi kwa mazoea na wamehusika kwenye vitendo ambavyo ni kinyume na maadili, tutawachukulia hatua kali kwa sababu wanaharibu taswira ya sekta ya Afya,"amesema Dkt. Magembe.

Aidha Dkt. Magembe amekemea vitendo vya utoroshwaji wa wagonjwa na kuwasababishia wananchi gharama zisizo za lazima huku akisisitiza hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kila atakaebainika.

“Zipo taarifa za baadhi yenu kutorosha wagonjwa kupeleka kwenye hospitali za nje badala ya kuendelea kupata huduma kwenye hospitali za umma na hivyo kuwasababishia wananchi usumbufu na gharama zisizo za lazima, tutashuhulika na wewe,"amesema Dkt.Magembe.

Hata hivyo Dkt. Magembe amewasisitizia watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kila mmoja awe tayari kujifunza mazuri kutoka kwa mwenzie ili wote wafanye kazi iliyo nzuri.

"Ni imani yangu hatutasikia wala kuona uzembe wa aina yoyote, bali mtabadilika na kufanya kazi zenu kwa bidii, ubunifu na uweledi mkubwa ili kutimiza malengo ya Serikali ya awamu ya sita ya kutoa huduma bora kwa wananchi wake,"amesisitiza Dkt.Magembe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news