Waziri Mkuu ashiriki maziko ya aliyewahi kuwa DC na Mbunge Fatma Mikidadi

LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 12 Novemba, 2023 ameshiriki maziko ya Bi. Fatma Mikidadi yaliyofanyia mkoani Lindi.


Bi.Fatma aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa nyakati tofauti. Mheshimiwa Majaliwa amesema Bi. Fatma ni miongoni mwa viongozi wa awali wa Wilaya ya Ruangwa ambao wameacha alama kubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Amesema, enzi za uhai wake alikuwa miongoni mwa watu waliofanya jitihada kubwa ya kuhakikisha Mkoa wa Lindi unapata maendeleo kwa kushiriki katika miradi ya kuwainua wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news