Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kupunguza kiwango cha umaskini

JOSEPH MAHUMI NA FARIDA RAMADHANI
WF

WIZARA ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha nchini wameandaa Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (katikati), akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya 3 ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini, yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha. Kulia ni Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Noves Moses na Kushoto ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Arusha, Bi. Grace Masambaji.

Hayo yameelezwa jijini Arusha na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini humo.

Alisema kutokana na Utafiti wa FinScope wa mwaka 2023 nchini, ni asilimia 53.8 tu ya nguvu kazi wanatumia huduma rasmi za fedha ambapo kundi kubwa la Watanzania halifaidiki na huduma hizo hivyo kukosa fursa za kuboresha maisha yao kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zingewawezesha kuchangia katika kukuza Pato la Taifa.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akizungumza na wanahabari kuhusu Kitaifa yatakayotoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutumia huduma rasmi za fedha ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza kiwango cha umasikini nchini, yatakayofanyika tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

“Serikali inakusudia ifikapo mwaka 2025 takriban asilimia 80 ya wananchi watakuwa wamepata uelewa wa masuala ya fedha ikiwemo benki, bima na mifuko ya uwekezaji”, alibainisha Dkt. Mwamwaja.

Alisema maadhimisho hayo ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 ambapo elimu kwa umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa Mpango huo.

“Madhimisho hayo pamoja na mambo mengine yanalenga kuwajengea wananchi uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za fedha, fursa zinazopatikana katika Masoko ya Fedha kupitia elimu ya fedha pamoja na namna bora ya kusimamia fedha”, alisema Dkt. Mwamwaja.

Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwaunganisha wananchi, wajasiriamali na wadau wengine ili waweze kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na sekta ya fedha katika kukuza na kuimarisha biashara zao
Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bi. Noves Moses, akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, ambapo Benki Kuu pamoja na taasisi zingine za fedha zitashiriki ili kutoa elimu ya fedha kwa wakazi wa mkoa wa Arusha katika viwanja vya vya Sheikh Amri Abeid, jijini humo, kuanzia tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023.

Aidha, aliwakaribisha wananchi wa Arusha na mikoa ya jirani kushiriki maadhimisho hayo ambayo yanafanyika bila kiingilio chochote.

Kwa upande wa wadau wengine ambao watashiriki kutoa elimu na huduma katika maadhimisho hayo wamesema kuwa maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na wapo tayari kutoa huduma.
Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Arusha, Bi. Grace Masambaj, akizungumza na wanahabari akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, ambapo vyama vya ushirika vya kifedha (Saccoss) vitashiriki katika maonesho hayo kutoa elimu na ushauri kwa wakazi wa mkoa wa Arusha, na maeneo mengine nchini wakaohudhuria kwenye Maonesho hayo, katika viwanja vya vya Sheikh Amri Abeid, jijini humo, kuanzia tarehe 20 hadi 26 Novemba, 2023.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa siku ya Jumatano ya tarehe 22 Novemba, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news