KAGERA-Wakala wa Vipimo (WMA) imeandaa na kutoa semina kwa kamati ya kudumu ya Bunge ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoa wa Kagera kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu kazi na majukumu ya wakala huo.


.jpeg)
"Sisi kama kamati ya Bunge tunaosimamia na kuishauri Serikali tunnailekeza Wizara kuwa na zoezi endelevu la ukaguzi wa vipimo sahihi sambamba utoaji elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipimo hasa kwa wananchi wa chini ambao ndio walaji wa mwisho ili kuhakikisha kiasi cha fedha wanacholipa kiendane na kiasi cha bidhaa wanazonunua,"amesema Mwanyika.


.jpeg)


.jpeg)


Bi. Stella ameeleza kuwa Wakala wa Vipimo ina ofisi katika mipaka mbalimbali Mutukula ukiwa ni mmoja wa mipaka hiyo ikiwa na lengo la kuhakiki usahihi wa bidhaa zote zinazoingia nchini kupitia mipakani ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia zinakuwa sahihi wakati wote kwa lengo la kuwalinda walaji na amesisitiza kuwa Wakala itaendelea kufungua ofisi kwenye mipaka mipya itakayoendelewa kufunguliwa kwa ajili ya kuwalinda walaji kwa kukagua mizigo itakayopita kwenye mipaka hiyo ili iwe kwenye vipimo sahihi.
Tags
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Habari
Kamati ya Bunge
Kamati za Bunge
Wakala wa Vipimo (WMA)