Ajali yaua wanne, yajeruhi 21 Kagera

KAGERA-Watu wanne wamekufa na wengine 21 kujeruhiwa katika ajali iliyosababishwa na gari lenye usajili namba T 339 DBV aina ya Toyota Hiace.

Gari hilo lilikuwa likitokea Izimbya Bukoba Vijijini kuelekea Bukoba Mjini mkoani Kagera. Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda.

Amesema, tukio hilo lilitokea majira ya saa tano asubuhi Desemba 5, 2023, maeneo ya Kyetema katikati ya Kata za Kemendo na Bujugo Halmashauri ya Bukoba.

Kamanda Chatanda amesema, waliopoteza maisha ni watu wazima watatu na mtoto mmoja, huku kati ya majeruhi 21 watoto ni wanne watu wazima 17, ambao walikimbizwa Hospitali ya Bujuna Ngoma ambayo ni ya wilaya hiyo.

Amesema, kutokana hali ya majeruhi wengi kuwa mbaya, wengine wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.

Hata hivyo, Kamanda huyo amesema, uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni mwendo kasi ambapo dereva alishindwa kulimudu gari kwenye mteremko likaenda kugonga nguzo za umeme pamoja na pikipiki zilizokuwa kwenye maegesho ya barabara maeneo hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news