Amani ni nguzo muhimu nchini-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa na baadae kushiriki Dua Maalum ya kumuombea iliyoandaliwa na Jumuiya ya Fysabilillah Tabligh Markaz Zanzibar Msikiti wa Mwembe Shauri, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema, siasa zimetulia, amani ipo, watu ni wamoja tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aidumishe amani iliyopo , umoja na mshikamano kwa watu na upendo.

Pia ameushukuru Uongozi wa Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar kwa uratibu mzuri wa shughuli za dini nchini.

Hafla hiyo ya Desemba 15,2023 imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali , Chama Cha Mapinduzi na dini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news