Bodi na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakutana na ZHC

ZANZIBAR-Bodi na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo imekutana na Menejimenti ya Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) ili kufahamiana na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuwahudumia watanzania wa pande zote za Muungano katika sekta ya nyumba.
Wajumbe wakipata maelezo ya utekelezaji wa mradi eneo la Mkunazini kwa Injinia Mchanga Ali Mohamed jijini Zanzibar.
Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Dkt. Sophia Kongela ameishukuru Bodi na Menejimenti ya ZHC kwa mwaliko wao na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta ustawi wa wananchi wanaohudumiwa na mashirika hayo mawili.
NHC imeshiriki mara kwa mara kutoa mafunzo kwa ZHC ya namna ya kuendesha Shirika hilo la nyumba ili kuleta tija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news