Makumi wahofiwa kufariki ajali ya basi la Mkombe Luxury kutoka Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam,Tanzania

SERENJE-Makumi ya watu wanahofiwa kufariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kutokana na ajali iliyohusisha basi la Mkombe Luxury ambalo limegongana na Lori maeneo ya Serenje nchini Zambia.

Serenje ni mji wa Wilaya ya Serenje, Zambia, ulio karibu na Barabara Kuu ya Kaskazini na Reli ya TAZARA.

Aidha,Serenje iko takriban kilomita 191 kutoka Kapiri Mposhi kwenye Barabara Kuu ya Kaskazini.
Basi hilo ambalo huwa linafanya safari za moja kwa moja kutoka jijini Johannesburg hadi Dar es Salaam lilikuwa linakuja nchini Tanzania.

"Ajali imetokea, hivyo wana familia kama wana ndugu walikuwa wanasafiri kutoka South Africa kwenda Tanzania na Bus la Mkombe Luxury please jaribuni kuwatafuta.

"Maana limepata ajali mbaya sana ya kugongana na Lori muda huu hapo Serenje Zambia."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news