Dar yakutanisha wanawake kutoka mataifa 54 barani Afrika,Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt.Samia

DAR ES SALAAM-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 6, 2023 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kongamano la Pili la Wanawake katika biashara ndani ya Eneo huru la Biashara Africa (AfCFTA) linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kongamano hili la Wanawake katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika, ni Kongamano la pili kufanyika ambapo Kongamano la Kwanza lililofanyika tarehe 12-14 Septemba 2022 jijini Dar es Salaam ambalo lilihudhuriwa na washiriki wapatao 1060 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwemo viongozi wananwake katika ngazi mbalimbali. 

Kongamano hilo lililenga kuwakutanisha Viongozi Wakuu Wanawake, Mawaziri, Wanawake Wajasiriamali na wadau wengine ili kujadili, kutoa maoni, ushauri na mapendekezo ya kuwezesha uandaaji wa Itifaki kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake na Vijana kushiriki kikamilifu katika biashara ndani ya AfCFTA.
Mafanikio makubwa yaliyotokana na Kongamano la kwanza la mwaka 2022 ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kupata maazimio yaliyowezesha kuandaa na kukamilisha Rasimu ya Itifaki ya Wanawake na Vijana katika Biashara ndani ya AfCFTA ambayo kwa upande wa Tanzania iko katika hatua mbalimbali za kuridhiwa ili iannze kutumika nchini

Pamoja na kufanikiwa kwa itifaki hiyo, Kongamano hilo lilitoa njia sahihi za kutatua vikwazo na changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na vijana katika biashara ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika biashara barani Afrika, ikiwa ni pamoja na upatikanaji mdogo wa fedha, taarifa za masoko, pembejeo, matumizi ya teknolojia, masoko, uwezo mdogo wa kufuata viwango na mahitaji mengine ya kisheria.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news