Hivi ndivyo Nabii Bilionea Rev.Lucy Natasha alivyotua Dar, kugawa mitaji RGC Miracle Centre Tabata

NA DIRAMAKINI

HATIMAYE Nabii Bilionea Rv.Lucy Natasha yupo jijini Dar es Salaam ambapo atahudumu kwa siku tatu katika Kongamano Kubwa la Majira Mapya ndani ya RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe.

Kupitia kongamano hilo, mbali na Rev.Lucy Natasha pia ameambatana na Bishop Innocent Rugagi kutoka nchini Rwanda.

Akizungumzia kuhusu ujio wa ugeni huo mzito, Balozi wa Amani Duniani na Mtume wa Urejesho, Dkt.Peter Nyaga amesema, kongamano hilo linaanza leo Desemba 1, 2023 na Jumapili ya Desemba 3, 2023 Nabii Rev. Natasha atagawa mitaji kwa wajasiriamali mbalimbali.

Pia, kongamano hilo ambalo linatarajiwa kwenda sambamba na sherehe za miaka 17 ya Huduma ya Urejesho, mbali na mitaji pia watu mbalimbali weenye mahitaji maalum katika jamii watagawiwa misaada vikiwemo vyakula.

“Tunashukuru tena kupata nafasi ya kumleta Nabii mwanamke wa Oracle of God, Rev.Lucy Natasha ambaye siyo mara ya kwanza kuwa Tanzania,mwaka jana alikuwa hapa na tena amerudi kabla ya mwisho wa mwaka.Ninajua kwamba, kitaeleweka…Rev.Natasha karibu sana Dar es Salaam.”
Kwa upande wake Rev. Lucy Natasha amesema kuwa, “Nichukue nafasi hii kwanza kuwashukuru kwa mapokezi ya leo, ndiyo tumefika hapa Dar es Salaam, Tanzania na mwaka huu hii ndiyo mara ya kwanza kufika Dar es Salaam tena.

“Mwaka huu wa 2023 na tumekuja kwa ajili ya kongamano kubwa na kongamano hili ni kongamano la watu wa madhehebu yote wanakaribishwa, mkutano huu ni mkutano ambao utabadilisha maisha yako.

“Pale RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe kumbuka Mungu anapotuma Nabii anatuma Nabii kwa ajili ya faida yako, a prophet come to prophesize you, a prophet come to accelerate you, hivyo ninachukua nafasi hii kuwakaribisha Watanzania wote na watu wa dhehebu zote.

“Chochote ambacho unaamini Mungu akufanyie, hili ni kongamano la kumiliki na kutawala ni kongamano la uponyaji na vile vile tutaunganika pamoja na mtumishi wa Mungu ambaye ametoka Rwanda,Bishop Innocent Rugagi na ninamshukuru mwenyeji wetu Apostle Peter Nyaga pamoja na Apostle Muliri kwa kutupokea siku ya leo, Watanzania mjiandae tunamaliza mwaka huu na ushuhuda.

“Tumekuja kuachilia neema na upako, ambao utakupeleka kiwango kingine, nichukue nafasi hii kuwakaribisha wafanyabiashara wote, wanandoa wote, wote wanaoamini Mungu awapatie kibali na wote ambao wanataka neema ya kumtumikia Mungu.

“Tumetumika kwa nchi zaidi ya 50 duniani kote na tumekuja kwa ajili ya kuwaambia Watanzania wakati umefika wa kumtumikia Mungu, hivyo wote mnarakibishwa, Mungu awabariki sana.

“Na pia tumpongeze Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muunhgano wa Tanzania) kwa ajili ya kualika Afrika yote hapa na kufanya sisi wa hapa nchi jirani tunajisikia tuko nyumbani tukifika Tanzania.

“Kwa hiyo Mama Samia tunakupenda na kama mwanamke tunajivunia wewe sana, na wanawake wote wa Tanzania mjitambue na tufuate mfano wa Mama Samia Suluhu, mbarikiwe sana Watanzania, tunawapenda na tunategemea kuwaona kwenye hili kongamano RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. I see your face, I see your case, I see your case, I prophesize, God Bless you.”

































Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news