Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha awapongeza wachezaji mabao 3-0 kwa Kagera Sugar

DAR ES SALAAM-Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amewasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Ni katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Desemba 15,2023 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Benchikha amesema uwanja, haukuwa rafiki na kuwanyima kucheza soka safi, lakini hata hivyo amefurahi kwa ushindi huo mnono.

Aidha,Benchikha amesema Kagera Sugar ni timu nzuri na waliwapa ushindani mkubwa, lakini walikuwa bora na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.

“Tumecheza vizuri, nawapongeza wachezaji wangu. Tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi

“Kagera ni timu nzuri wanacheza soka safi na walitupa ushindani mkubwa ingawa sisi tulikuwa bora ndio maana tumepata ushindi,” amesema Benchikha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news