Simba SC yaichapa Kagera Sugar mabao 3-0 Ligi Kuu ya NBC

DAR ES SALAAM-Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Uwanja wa Uhuru ulimalizika kwa Simba SC kupata ushindi wa mabao 3-0.
Kupitia mtanange huo ambao umepigwa Desemba 15,2024 Simba SC walianza mchezo kwa kasi huku wakitengeneza nafasi.

Aidha,kikwazo kikubwa kwa Simba SC kilionekana ni mlinda mlango wa Kagera, Ramadhani Chalamanda.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi wa kati, Denis Bukenya.

Kipindi cha pili Simba SC waliongeza kasi na kuzidi kufika zaidi langoni mwa Kagera, lakini mashambulizi yake mengi yaliishia kwa Chalamanda.

Sadio Kanoute aliwapatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 75 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la tatu dakika ya 90 baada ya kutumia makosa yaliyofanywa na mlinzi Abdallah Mfuko kurudisha mpira kwa mlinda mlango kabla ya kuiwahi na kumfunga kirahisi Chalamanda.

Huu ni mchezo wa kwanza wa ligi kwa kocha Abdelhak Benchikha kukiongoza kikosi cha Simba SC huku wakipata ushindi mnono bila kuruhusu bao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news