MAAFA KATESH:Ufunguaji wa mitaa wafikia asilimia 85, Serikali yaahidi

MANYARA-Serikali imesema zoezi la ufunguaji wa mitaa katika mji wa Kateshi limefika 85% na mkazo mkubwa umewekwa katika kutoa udongo kwenye vipenyo vya vya mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika maeneo tofauti akiongoza zoezi la urejeshaji wa hali katika Mji wa Katesh katika Halmashauri ya Hanang’ mkoani Manyara.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama katika mahojiano maalumu aliyoyafanya na Shirika la Utangazaji la Taifa TBC tarehe 13 Desemba, 2023 wilayani Hanang' mkoani Manyara.

Waziri alisema katika zoezi hilo malori makubwa zaidi ya 30 yalisaidia kutoa tope lenye mawe miti pamoja na udongo, katika barabara kuu ya Katesh Singida.

“Malori yenye uwezo wa kubeba magunia 130 yamefanya safari zaidi ya 400 ya kutoa Tope kutoka kwenye viunga vyote vya Mji wa Katesh,” alibainisha.

Waziri amefafanua kwamba, vifaa tulivyonavyo haviwezi kuingia kwenye vipenyo vya mtaa kwa mtaa au nyumba kwa nyumba na hivyo tunalazimika kutumia nguvu kazi, na tunafanikiwa.
Halikadhalika tunafikiria kushirikisha wananchi kujitokeza kusaidia zoezi la uondoaji wa tope hasa kwenye hifadhi ya barabara ili tuweke hali katika usalama zaidi.

“Tunafanya tathimini na kuendelea kuchukua tahadhari mvua nyingine ikinyesha, ikiwa ni pamoja na kurudisha mto uliopokea mawe na matope ambao njia yake ilifunga na kutengeneza mapito mengine,”alifafanua.
Kwa upande wake Mkazi wa Katesh, Bi, Halima Rashidi amesema Mawe na tope yaliyoletwa na Mlima Hanang yaliathiri kwa kiasi kikubwa miundo mbinu na makazi ya watu.

“Msaada wa serikali umekuja kwa wakati na haraka, watu wana moyo wa kufanya kazi kwa sababu jitihada zao zimeokoa maisha ya watu na mali,” alibainisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news