MAAFA KATESH:TFRA,wadau wa mbolea nchini watoa msaada

MANYARA-Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent, amekusanya kiasi cha tani 78.5 za mbolea zenye thamani ya shilingi Milioni 129,449,094 kutoka kwa wadau wa mbolea zitakazokabidhiwa kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyotokea wilayani Hanang, katika mji mdogo wa Katesh hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent (wa tatu kutoka kushoto) akipokea kiasi cha tani 30 za mbolea za kupandia na kukuzia kutoka kampuni la Uzalishaji wa Mbolea Itracom ya Nala jijini Dodoma.

Laurent amekabidhiwa kiasi cha tani 65 za mbolea za kupandia na kukuzia leo tarehe 7 Desemba, 2023 zilizotolewa na wazalishaji na wafanyabiasha wa mbolea nchini.

Amepokea tani 30 za mbolea kutoka Kampuni ya Mbolea yaa Taifa (TFC), tani 30 kutoka Kampuni ya Uzalishaji wa Mbolea Itracom na kiasi cha tani 5 kutoka Kampuni ya Mbolea na Uchimbaji madini Minjingu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent (wa pili kulia) akikabidhiwa mbolea kiasi cha tani 30 na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC), Samuel Mshote (Wa pili kushoto).

Aidha, Laurent ameeleza kuwa, anataraija kupokea mbolea za misaada kutoka kampuni ya Mbolea la Staco tani 10, Yara tani 2.5 na tani 1 kutoka kampuni ya mbolea ya Premium.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent (katikati) akikabidhiwa mbolea kutoka kwa Afsa ugani na masoko wa kiwanada cha mbolea Minjingu, Frank Felix Kamhabwa katika kituo cha kilimo kilichopo katika mji wa Katesh wilayani Hanang leo tarehe 7 Desemba, 2023.

Amesema, milango iko wazi kwa wadau wa mbolea kufikisha misaada yao itakayowasaidia waathirika wa mafuriko wakati huu wa msimu wa kilimo kutokana na kuwa wakulima walikuwa wamenunua mbolea ambazo hazijazaa matunda kutokana na athari za mafuriko walizokutana nazo.
Akizungumzia hali ya usajili kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku, Laurent amesema, wakulima 8449 wa Hanang' wamejiandikisha na walishanunua kiasi cha tani 1,131.2 za mbolea mpaka wanapopata majanga haya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news