Mheshimiwa Pauline Gekul afutiwa kesi, Wakili Madeleka asema hawakubali

MANYARA-Mahakama ya Wilaya ya Babati, mkoani Manyara imeifutilia mbali kesi ya ukatili iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Babati Mjini, Mheshimiwa Pauline Gekul.
Ni kuhusu tuhuma za unyanyasaji kwa kijana Hashim Ally.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Babati, Victor Kimario ametoa uamuzi huo leo Desemba 27, 2023.

Amesema, amefuta kesi hiyo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa kupitia kwa Wakili Peter Madeleka chini ya kifungu cha 128 (2) na (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Kwa upande wake Wakili Madeleka amesema, hawajakubaliana na maamuzi hayo na kwamba watakata rufaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news