Michael Lushinge Masanja (Smart) ashinda uenyekiti CCM Mkoa wa Mwanza

MWANZA-Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kimepata mwenyekiti mpya ambaye ni ndugu Michael Lushinge Masanja maarufu kama Smart.

Masanja amechaguliwa kwa kura 784 kati ya 1,111 na kuwashinda wagombea wenzake wanne waliopata kura 299 kwa pamoja huku kura 28 zikiharibika.

Uchaguzi huo umefanyika Desemba 4,2023 kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Sixbert Ruben aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Said Mtanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara ndiye aliyesimamia uchaguzi huo ambapo wakati akitangaza matokeo amesema, wagombea walikuwa ni Michael Lushinge Masanja (Smart),David Mayala Mulongo, Sabana Lushu Salinja, Elizabert Watson Nyingi na Dkt.Angelina William Samike.

Mtanda amesema, wajumbe waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 1,155 lakini waliopiga ni 1,111 kura 28 ziliharibika na kura halali zilikuwa 1,083 ambapo Michael Lushinge Masanja alipata kura 784 kati ya zilizopigwa.

Aidha, Sabana Lushu Salinja alipata kura 250, David Mayala Mulongo 20, Dkt.Angelina William Samike 15 na Elizabeth Watson Nyingi kura saba, hivyo akamtangaza Michael Lushinge Masanja kuwa mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news