NBAA yawafikia watoto wanaougua saratani Muhimbili

DAR ES SALAAM-Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa hundi yenye thamani shilingi milioni 15 kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaougua saratani wanaopatiwa matibabu hospitalini hapa.
Akipokea msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Julieth Magandi amesema matibabu ya saratani yanagharama kubwa hivyo jamii haina budi kuchangia huduma na kwa wale wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia wenye uhitaji ili huduma hizi ziwe endelevu.
Amesema,hospitali inawahudumia watoto wenye saratani ambao wengine wanaishi ndani ya hospitali kutokana na matibabu yao kuchukua muda mrefu.

‘‘Ninatoa wito kuwasaidia wenye uhitaji kwani matibabu ya kibingwa yanagharama kubwa.

"Natumia fursa hii kutoa wito kwa jamii kujiunga na bima ya afya ili kuweza kumudu gharama za matibabu,’’ameeleza Dkt. Magandi.
Awali akizungumza kabla ya kukabidhi hundi , Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, CPA Pius Maneno amesema kila mwaka wana utaratibu wa kurejesha kwa jamii kwa mwaka huu wameona ni vema wakawagusa watoto wanaoumwa saratani ambao wamelazwa Muhimbili.

‘’Nimesimama hapa kuwawakilisha wahasibu na wakaguzi wa Tanzania, tunaahidi kuendelea kushirikiana na MNH katika kuboresha utoaji wa huduma za afya, pia tunapongeza mabadiliko makubwa yaliyofanyika Muhimbili najua hii ni juhudi ya Serikali ya kuboresha huduma za afya pia haya yote yamefanikiwa kutokana na uongozi mzuri wa Muhimbili,’’amesema CPA Maneno.
Naye Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Muhimbili CPA Ashraph Abdulkarim ameishukuru NBAA kwa msaada huo na kuomba bodi zingine kuguswa na kujitokeza kuchangia huduma za afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news