Rais Dkt.Mwinyi afungua Mkutano wa Benki ya Dunia wa IDA20 Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imeweka kipaumbele kwa kuongeza uwekezaji katika elimu, afya, na huduma nyingine za kijamii pamoja na kilimo kinachozingatia hali ya hewa na mazingira.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan alipofungua Mkutano wa Kimataifa wa Tathmini ya muda wa kati wa mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia(IDA20 Mid Term Review) unaofanyika hoteli ya Golden Tulip uwanja wa ndege, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 06 Desemba 2023.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Pia kwa kuongozwa na falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Samia Suluhu Hassan inayohusu mambo manne ya msingi ya kuzingatiwa ambayo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na ujenzi mpya.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema uchumi wa Zanzibar unanufaika na utalii wa kitamaduni ikiwemo Mji mkongwe ambao ni eneo la urithi wa dunia .

Vilevile Zanzibar ilipata msaada kutoka IDA fedha za kigeni dola za kimarekani Milioni 93 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mijini na kuhifadhi mazingira ya urithi wa kitamaduni.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ametolea mfano wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi(COP28) huko Dubai, alisema Rais Dkt.Samia amejitolea kutetea ajenda ya kusaidia kupunguza nishati mimea ambayo huathiri mazingira alipoongoza uzinduzi wa mradi wa Nishati safi ya kupikia itakayowasaidia Wanawake Barani Afrika(AWCCSP) .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news