RAIS DKT.MWINYI ATEMBELEA MAKTABA YA TAIFA QATAR

DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi ametembelea Maktaba ya Taifa ya Qatar kwa mwaliko wa Waziri wa Nchi, Naibu Waziri Mkuu na Rais wa Maktaba ya Taifa ya Qatar, Mhe. Dk. Hamad bin Abdulaziz Al-Kawari tarehe 9 Desemba 2023 Doha, Qatar.
Baadae Rais Dkt.Mwinyi alizungumza na Mhe. Dkt.Hamad bin Abdulaziz Al-Kawari ambapo aliwaalika wafanyabiashara wa Qatar na hasa wawekezaji wa nishati kuja Zanzibar kuwekeza.

Pia aliwaombea nafasi vijana wa Kizanzibari kuja Qatar kujifunza masuala ya uendeshaji wa maktaba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news