Rais Dkt.Samia afanya uteuzi TMA, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Bodi ya Mkonge

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Bodi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 13, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Jaji Mshibe Ali Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (Tanzania Meteorological Authority – TMA).

Vile vile, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Dkt. Emmanuel Jonathan Mpeta kuwa Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Balozi Adadi Mohamed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na amemteua Bi. Fatma Mohamed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Theobald Maingu Sabi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge, Tanzania. Uteuzi huu umeanza Desemba 10, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news