Rais Dkt.Samia aiagiza Serikali ielekeze nguvu zote katika maafa ya Katesh mkoani Manyara

ABU DHABI-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia maafa yaliyotokea Kijiji cha Katesh wilayani Hanang' mkoani Manyara.

Kutokana na maafa hayo ambayo yametokea leo Desemba 3,2023 na kusababisha vifo ikiwemo majeruhi na uharibifu wa miundombinu na mali, Rais Dkt.Samia amesema;
“Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kutokea kwa mvua kubwa Mkoa wa Manyara na kuleta madhara makubwa katika Kijiji cha Katesh, sisi tuliopo huku (Dubai) ambao tunashikiri mkutano wa mazingira tumesikitishwa sana na tukio hili, lakini mipango ya Mungu ndivyo inavyokwenda tunatoa pole kwa wahanga wa tukio hili.

“Nimeelekeza nguvu zote za Serikali zielekezwe huko kwenye uokozi na kuzuia maafa zaidi kutokea.

"Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama nimevielekeza vifike huko, Wizara ya Afya kushughulikia majeruhi, lakini pia Wizara ya Madini kuona nini kinatokea katika sehemu ambayo milima imeonesha kutetemeka au kuporomoka.

“Nimemtaka Waziri pia anayeshughulika na maafa awepo huko, niwape pole wananchi wote nami nipo njiani kurudi huko kuja kushirikiana na wananchi katika hili lililotupata,”amesema Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news