Serikali yatoa wito kwa wananchi kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutambua miili ya waliofariki katika ajali ya Mukombe Luxury iliyoua 13 na kujeruhi 43

DODOMA-Serikali imetoa wito kwa wananchi kufika katika Hospitali ya Taifa kwa ajili ya kutambua miili ya watu waliofariki katika ajali ya barabarani nchini Zambia.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 31,2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

"Serikali za Jamhuri ya Zambia zilitoa taarifa kuhusu ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria aina ya Volvo la Kampuni ya Mukombe Luxury lenye namba za usajili DK72 HH GP linalofanya safari kati ya Afrika Kusini na Tanzania lililogongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T850 DSN la nchini Tanzania.

"Ajali hiyo iliyotokea katika Wilaya ya Serenje, Jimbo la Kati nchini Zambia tarehe 26 Desemba 2023, ilisababisha vifo vya watu 13 na majeruhi 42 wa mataifa mbalimbali, ikiwemo Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Afrika Kusini, Botswana na Zambia.

"Watanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Bw. Oscar Mwamulima (37) mwenyeji wa Mbozi, Mbeya; Bw. Said Mohamed Dige (20) mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE403048, mzaliwa wa Ilemela, Mwanza; Bw. Peter Blass Munishi (48) mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE378465, mzaliwa wa Siha, Kilimanjaro;

"Bw. Bashiru Salum Kiluwa (42) aliyekuwa dereva msaidizi wa Basi mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE173695, mzaliwa wa Lushoto, Tanga; Bw. Rashid Athumani Salehe, Dereva wa Lori mkazi wa Tanga; na Hassani Abdallah Ramadhani, Utingo wa Lori mwenye Hati ya kusafiria Na. TAE667038 mkazi wa Muheza, Tanga.

"Miili ya Marehemu hao imetambuliwa na ndugu zao isipokuwa marehemu wawili, Bw. Said Mohamed Dige na Bw. Peter Blass Munishi. Ndugu wa marehemu hawa wanahimizwa kufika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutambua miili ya wapendwa wao,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news