Simba SC yatoka sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca

MARRAKECH-Wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC wametoka sare ya bao 1-1 kupitia mchezo wao wa tatu waliocheza na Wydad Casablanca.
Ni kupitia mtanange uliopigwa Desemba 9, 2023 katika Uwanja wa Marrakech nchini Morocco ambapo Simba SC walikuwa wageni huko.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu, lakini mechi ikichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Mlinda mlango, Ayoub Lakred alicheza mkwaju wa penati uliopigwa na nahodha, Yahya Jabrane dakika ya 41 baada ya Kibu Denis kumchezea madhambi Saifdine Bouhra ndani ya 18.

Kipindi cha pili Simba SC waliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini ufanisi wa kutumia nafasi zilizopatikana ulikuwa mdogo.

Zakaria Draoui aliwapatia wenyeji bao la ushindi dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jabrane.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news