VIDEO:Rais Dkt.Mwinyi ashiriki mdahalo wa Uchumi wa Kidigitali jijini Doha

DOHA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, mageuzi ya kidijitali Tanzania yamesaidia kufikiwa kwa huduma za kidijitali ikiwa ni pamoja na elimu na huduma za afya.

Hatua ambayo imesaidia kuboresha maisha ya watu, kuendesha soko shindani na ubunifu na kukuza ushirikishwaji.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika mdahalo wa mada isemayo: "Nchi yako iko tayari kujenga uchumi wa kidijitali?" katika jukwaa la Doha Forum lililowashirikisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Costa Rica, Mhe. Arnoldo Andre Tinoco, Rais wa Mamlaka ya Mawasiliano Qatar,Mhandisi Ahmad Almuslemani.

Wengine ni Afisa Mtendaji Mkuu na Muasisi wa Taasisi ya Descartes Institute for the Future, Mkurugenzi wa Masoko Google, Selim J.Edde, Mkuu wa Digitali UNDP, Keyzom Ngodup ukiongozwa na Mwandishi wa Kituo cha CNBC, Dan Murphy katika ukumbi wa Hoteli ya Sheraton Doha, Qatar leo Desemba 11, 2023.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa dunia inabadilika katika suala la matumizi ya kidijitali na Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika hazipaswi kuachwa nyuma.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua udhamira thabiti wa maono juu ya kuifikisha nchi kufikia malengo ya 4 ya dunia na Mapinduzi ya 5 ya viwanda yanayokuja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news