Wafamasia Muhimbili watunukiwa vyeti ufanyakazi bora

NA GRACE MTAWA

MAPEMA leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Julieth Magandi amewatunuku vyeti vya ufanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024, Wafamasia watano na Mteknolojia Maabara mmoja kutoka Kampasi ya Upanga na Mloganzila ili kutambua mchango na juhudi zao katika kutekeleza majukumu yao.









Dkt. Magandi ameipongeza Idara ya Famasi kwa kuwa na utaratibu mzuri wa kutambua wafanyakazi ikiwa ni mbinu mojawapo ya kutoa motisha na ari ya kufanya kazi kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi na utoaji huduma bora kwa wananchi.

Waliopata vyeti hivyo kutoka Mloganzila ni Mfamasia. Thomas Lukuba (Julai), Mfamasia. Keneth Kigobanya (Agosti) na Mfamasia. Biton Kigunga (Septemba) ambapo kutoka Upanga ni Mteknolojia Dawa. Mwanaheri Bafta (Julai), Mfamasia. Asukile Filemoni (Agosti) na Mfamasia. Rhoda Kahumba (Septemba).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news