Wakulima wa mwani waishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuwashika mkono

ZANZIBAR-Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar imepata bahati ya kutembelewa na Rais wa Benki ya Dunia,Ajaypal Singh Banga.
Rais huyo alifika mpaka Kijiji cha Muungoni kilichopo katika Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja ili kuwatembelea akina mama wa vikundi vya mwani kwa lengo la kuona maendeleo ambayo yamepatikana kupitia zao la mwani.

Kina mama hao wameeleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo katika ukulima wa zao hilo la mwani pamoja na kuishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuwashika mkono, kwani bado wanaendelea kunufaika na miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ikiwemo MACEMP na Mradi wa SWIOFish.

Ujio wa Rais wa Benki ya Dunia umeambatana na ufunguaji Mkutano wa IDA 20 MTR unaofanyika kwa siku tatu kuanzia 6-8 Desemba 2023 katika Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar ambapo mikutano hiyo inalenga kutoa ufadhili wa miradi ya maendeleo, sekta mtambuka pamoja na kusaidia nchi kuboresha matokeo ya utekelezaji wa miradi kwa maendeleo endelevu.

Aidha, Wizara ya Uchumi wa Buluu ni miongoni mwa wizara zinazoendelea kunufaika na ufadhili huo kupitia mradi ya MACEMP na SWIOFish amabayo ilitekelezwa kupitia Idara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini.

Sambamba na miradi iliyopita Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvivi inatarajia kunufaika na mradi mwengine mkubwa wa TASFARM ambao pia umelenga kuinua sekta ya uchumi wa Buluu na Uvuvi ikiwemo Kilimo cha Mwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news