Ujenzi Barabara Kuu ya Dunga kuelekea eneo la Viwanda waanza

ZANZIBAR-Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Barabara Kuu ya Dunga kuelekea eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda umeanza rasmi.

Ujenzi huo unafanyika chini ya Kampuni ya Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC).
Novemba 29, 2023 Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda ilitiliana saini na kampuni hiyo ili kuanza ujenzi huo katika eneo la Viwanda la Dunga Zuze.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban tarehe 5 Desemba 2023, alitembelea eneo hilo kuangalia hatua za awali za mradi huo, kisha kuzungumza na wananchi na kuwataka kushirikiana kikamilifu katika kulinda miundombinu ambayo ndio chachu katika kuleta maendeleo hapa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news