Watakiwa kumuunga mkono Prof.Muhongo ujenzi maabara shuleni

NA FRESHA KINASA

MKUU wa Wilaya ya Musoma Mkoa wa Mara Dkt. Halfan Haule amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Msongela Palale na madiwani wa Halmashauri hiyo, kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa juhudi anazozifanya za ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi katika shule za sekondari jimboni humo.
Dkt. Haule ameyasema hayo Novemba 30, 2023 katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika makao makuu ya Halmashauri hiyo katika Kata ya Suguti Wilayani humo.

Dkt. Haule amesema kuwa, Prof. Muhongo ameendelea kuonesha juhudi za dhati za kuchangia ujenzi wa Maabara katika shule za Sekondari jimboni humo. Hivyo Halmashauri na Madiwani wamuunge mkono Mbunge huyo kwa kutoa fedha za kuchangia ujenzi wa Maabara ili kulimaliza jambo hilo.

"Nikuombe Mkurugenzi na Madiwani wote tumuungeni Mkono Mheshimiwa Mbunge ambaye amekuwa mstari wa mbele kuchangia ujenzi wa Maabara za masomo ya Sayansi kila sehemu jimboni. Amekuwa akihangaika kutokana na dhamira yake njema aliyonayo kuhakikisha kila shule ya Sekondari inakuwa na maabara ili Watoto wasome kwa vitendo na kwa ufanisi.

"Kwa mfano Diwani wa Kata ya Bukumi Mheshimiwa Mnubi Mussa nilitarajia kusikia katika Kikao hiki cha baraza la madiwani ukimbana Mkurugenzi atoe fedha kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Maabara za Sayansi Mtiro Sekondari ambayo ipo kwenye kata yako lakini hoja hii sijasikia ukisema. ili tufike mbali madiwani na Mkurugenzi tuyapeni kipaumbele mambo haya ya msingi ambayo ni muhimu kwa Watoto wetu,"amesema Dkt. Haule.

Amesema kuwa, kuchangia ujenzi wa maabara hakuhitaji fedha nyingi kwa mkupuo bali hata kiasi kidogo Halmashauri inaweza kuwa inatoa kwa awamu. Na amehimiza Katika eneo ambalo Kuna nguvu ya mchango wa Mheshimiwa Mbunge na Wananchi Halmashauri iunge mkono kutoa fedha.

Aidha Dkt. Haule amepongeza wastani wa ufaulu wa asilimia 75 kwa matokeo ya darasa ya Saba yaliyotangazwa kwa Halmashauri hiyo. Ambapo imeshika nafasi ya sita kati ya Halmashauri tisa za Mkoa wa Mara na wastani kupanda kwa asilimia 8 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo wastani ulikuwa asilimia 67.9, jumla ya shule za Msingi 118, za serikali zikiwa ni 114, na binafsi shule 4.

Ameaisitiza mikakati ya pamoja baina ya Serikali, wadau na Wananchi jimboni humo unapaswa ifanywe kuhakikisha ufaulu unakuwa mzuri zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news