Waziri Mkuu azungumza na wanakijiji Chingumbwa

LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa leo Desemba 21,2023 amezungumza na wakazi wa Kijiji cha Chingumbwa katika kata ya Mbekenyera, Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza na wakazi wa kata hiyo Mheshimiwa Majaliwa aliwaeleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kushirikiana na Wana-Ruangwa na Watanzania wote katika kutatua changamoto zilizopo hivyo waendelee kuwa na imani naye.

Amesema kuwa, katika kipindi cha miaka miwili kata ya Mbekenyerea imepatiwa shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kwenye sekta za afya na elimu.

Aidha, amesema kuwa Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu ujenzi na ubora kwenye sekta ya elimu kuanzia shule ya msingi ili watoto wasitembee umbali mrefu kufuata shule.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news