Yanga SC yakaribia kileleni Ligi Kuu ya NBC, yaichapa Tabora United 1-0

DODOMA-Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imebuka na ushindi ugenini baada ya kuichapa bao 1-0 Tabora United kutoka mkoani Tabora.

Ni kupitia mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa Desemba 23, 2023 katika dimba la Jamhuri jijini Dodoma.

Mshambuliaji Stephane Aziz Ki dakika ya 21 ndiye aliyewapa ushindi waajiri wake kwa mpira wa faulo uliomshinda mlinda mlango wa Tabora United.

Klabu ya Yanga inafikisha alama 30 ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa imecheza mechi 11 huku Azam FC wanaendelea kukaa kileleni wakiwa na alama 31 wakicheza mechi 13.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news