Simba SC yapunguzwa kasi, yatoka sare ya mabao 2-2 na KMC FC

DAR ES SALAAM-Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC dhidi ya KMC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamanzi jijini Dar es Salaam umemalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Mchezo huo ulikuwa wa kasi na kuivutia huku Simba SC wakionekana kulimiliki sehemu kubwa, lakini hata hivyo hawakuweza kuzitumia.

Waziri Junior aliwapatia KMC bao la kwanza dakika ya 30 baada ya kumzidi ujanja beki Che Malone wa simba SC.

Said Ntibazonkiza awapatia Simba SC bao la kusawazisha dakika ya 58 kwa mkwaju wa penati baada ya Abdulkarim Mohamed kuunawa mpira ndani ya 18.

Aidha, Jean Baleke awatupatia bao la pili dakika ya 59 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Waziri Junior aliwafungia KMC bao la pili dakika ya 88 baada ya shuti kali lililopigwa na Tepsi Evance kutemwa na kipa Ayoub Lakred.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha alifanya mabadiliko yakuwatoa John Bocco, Willy Onana, Saido Ntibazonkiza, Sadio Kanoute na kuwaingiza Jean Baleke, Abdallah Khamis, Jimmyson Mwanuke na Luis Miqussone.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news