Bosi wa TARURA atoa agizo Morogoro

MOROGORO-Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Ndyamukama ameagizwa kuanza mara moja usanifu wa barabara ya Magole Estate-Mfuru pamoja na ujenzi wa mifereji ya maji katika mji wa Kilosa.
Agizo hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya barabara na mifereji ya maji iliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani hapa ambapo katika ukaguzi huo aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi.

Katika Kata ya Kitete walijionea uharibifu wa Barabara ya Magole Estate-Mfuru yenye urefu wa Km. 4.5 na Kata ya Mbuni walijionea mfereji wa maji unaosababisha mafuriko ya maji maeneo ya mjini.
Hata hivyo, Mhandisi Seff aliwataka wananchi wa mji wa Kilosa kuunda vikundi vya kijamii kwa ajili ya kufanya kazi za kusafisha barabara na mifereji ili waweze kutunza miundombinu wanayojengewa na Serikali lakini pia kuwaongezea vipato na kuondokana na umaskini.

Naye, Diwani wa Kata ya Mbuni, Shabani Maringo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa ujenzi wa mifereji ya maji katika mji wa Kilosa ambayo imepunguza madhara ya mafuriko kwa kiasi kikubwa katika mtaa wa Viwandani,Madaraka, Mjini, Makaburini na Shule ya Msingi Kichangani.
Amesema, athari wanazopata sasa zinatokana na maji yaliyoelekezwa kutoka kwenye matoleo ya maji ya mradi wa SGR na kuiomba TARURA kujenga mifereji mingine ili kuyachepusha maji hayo yanayozidi kwenye mfereji wa awali pamoja na kumalizia ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 750 uliochimbwa kwa nguvu za wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news