Lukas Paul Tarimo anayetuhumiwa kumchoma Beatrice James Minja visu afariki

KILIMANJARO-Siku chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kusema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice James Minja, Lukas Paul Tarimo ambayo aliyafanya huko Tarekea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, naye mtuhumiwa huyo amefariki.Mtuhumiwa Lukas Paul Tarimo anadaiwa kutekeleza mauaji hayo Novemba 12, 2023 na kukimbia kusikojulikana.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP David Misime tarehe 31 Desemba,2023 alieleza kuwa,  baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi lilianza mara moja uchunguzi kumtafuta aliyefanya tukio hilo ambapo mapema Desemba 31,2023 jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata.

SACP Misime alisema kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa mafichoni huko Kijiji cha Jema kilichopo Kata ya Olondonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.
Alibainisha kuwa, baada ya mtuhumiwa kuhisi atafikiwa na mkono wa sheria alijaribu kunywa sumu ya kuuwa wadudu, lakini jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo mtuhumiwa huyo na jitihada za kumkimbiza katika kituo cha afya zilifanyika ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubiri taratibu za kisheria.

Hata hivyo, leo Januari 2,2024 Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwa, Lukas Paul Tarimo amefariki;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news