Fahamu kwa nini Muhimbili haijawahi kutoa tangazo la uongezaji makalio,Prof.Janabi ataja mambo 12

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Prof. Mohamed Janabi ametaja sababu 12 kuhusu taarifa ya kuongeza makalio.
Hayo yanajiri ikiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila wameanzisha huduma ya puto na kupunguza wale wenye uzito mkubwa kuanzia kilo 90 kwenda juu na haijawahi kutoa tangazo rasmi la uongezaji makalio.

Hizi hapa sababu 12 za kwa nini uongezaji makalio si jambo la dharura, ungana na Prof.Janabi hapa chini;

1. Ni procedure maarufu duniani.

2. Ni elective procedure yaani sio emergency dharura. Ni maamuzi binafsi ya mtu. Kuwa siridhiki na muonekano huu nataka huu.

3. Procedure hii haihitaji mtambo maalum ni ultrasound machine kukupa muongozo sindano yako inapokwenda.

4. Madhara (maaumivu pale sindano itakapo pigwa) na kidonda kidogo pale palipo chanwa 2-3 cm.

5. Jina lake la kitaalam ni Brazilian Butt Lift.

6. Muhimbili haijawahi kutoa tangazo la marekebisho ya makalio.

7. Tangazo official la MNH lilikuwa la puto na kupunguza wale wenye uzito mkubwa 90 kwenda juu.

8. Wanufaika wa kupunguza uzito kwa njia hii waliofanyiwa na wako salama ni karibu 200.

9. Ina maana gani hawa watanzania wangeenda Uturuki, SA inakadiriwa ni $15,000 ukizidisha mara 200 hizo ni $3,000,000. Zimeokolewa kwenda nje ya nchi. Madaktari wetu wapata ujuzi maana tumefanya pamoja na Profesa mbobezi kutoka India.

11. Je MNH ina mpango wa kufanya Brazilian butt lift, Breast Augumentation na breast reduction? Jibu ni ndio kabla ya mwezi wa 6 2024.

12. MNH ni hospitali bobezi ni muhimu kufanya procedures tofauti na hospitali ndogo. Faida tutapunguza fedha chache za kigeni kwenda nje, tutawapa nafasi wataalamu kwenda na vitu walivyojifunza na kuleta wageni kutoka nje=Medical Tourism.

Hizi ndio Facts kutoka MNH🙏🏿

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news