Luteni Jenerali mstaafu, Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile afariki

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema, amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Luteni Jenerali (mstaafu), Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Luteni Jenerali (Mstaafu), Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha yake na utumishi wake kwa nchi yetu kama Mwanajeshi, Balozi na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (1983 - 1988).

"Tutamkumbuka pia kwa kujitoa kwake katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, kama mmoja wa askari wetu waliofundisha katika Jeshi la FRELIMO kabla na baada ya uhuru wa Msumbiji.

"Natoa pole kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda, wanajeshi wetu wote, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news