Maafisa Elimu nchini watoa milioni 20 kwa waathirika wa maafa Hanang'

DAR ES SALAAM-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amekabidhi Sh.Milioni 20 kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe.Jenista Mhagama kutoka kwa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mkoa na Halmashauri zote nchini kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Hanang' mkoani Manyara.
Mhe. Mchengerwa amekabidhi fedha hizo leo Januari 9, 2024 kwa Waziri Jenista katika Ofisi yake ndogo jijini Dar es Salaam, ambapo amepokea fedha hizo kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mchengerwa amesema, fedha hizo zilitolewa kwenye Mkutano wa Maafisa Elimu hao mwishoni uliofanyika Manispaa ya Morogoro ambapo Maafisa hao wametoa mchango wao kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwahudumia wananchi wa Hanang waliopatwa na maafa ya maporomoko ya mawe na tope.

"Maafisa Elimu kwa ushirikiano wao waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang na kunituma nikukabidhi wewe Mhe.Waziri mwenye dhamana,"amesema.

Naye, Waziri Mhagama amewashukuru kwa mchango huo na kuunga mkono serikali katika kuhudumia wananchi hao na kwamba fedha hizo zimewekwa kwenye Akaunti ya maalum ya maafa iliyoko Benki Kuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news