Waziri Makamba:Tanzania katika eneo la kidiplomasia ina sifa na hadhi ya kipekee duniani

DAR ES SALAAM-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amesema Tanzania katika eneo la kidiplomasia ina sifa na hadhi ya kipekee duniani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.

Waziri Makamba ametoa kauli hiyo akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Januari 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) akifunga Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.

"Ili nchi iweze kufanya mambo yake vizuri duniani, lazima iwe na ushawishi mkubwa duniani, na Tanzania ni moja ya nchi zenye ushawishi mkubwa duniani,” alisema Waziri Makamba.

Aliongeza kuwa Nchi au Kiongozi lazima ilinde utu, uhuru wake duniani na hayo yote yataonekana kupitia Sera ya Mambo ya Nje.

“Kupitia Sera ya Mambo ya Nje, nchi inapata kukuza uwezo wa kujiamulia mambo yake, na kujipambanua jinsi ambavyo itaendesha mambo yake,”9
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Bakari Machumu akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia kufanyiwa marekebisho kwa Sera hiyo, Waziri Makamba amesema marekebisho hayo yamelazimika kufanyika kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea duniani kwa wakati huu na hivyo kuilazimu Tanzania kuendesha mambo yake kwa mujibu wa mabadiliko hayo.

Ametaja mabadiliko hayo kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi, kuibuka kwa taasisi zenye nguvu, ushawishi na uwezo wa kubadilisha vitu duniani, maendeleo ya teknolojia ya Habari na mawasiliano na uwepo wa asilimia kubwa ya watanzania waliozaliwa baada ya mwaka 2001 wakati sera hiyo ilipotengenezwa.
Mwanasisa Mkongwe, Prof. Anna Tibajaijuka akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Bishara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi John Ulanga akiendesha mjadala wakati wa Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.

Amesema kutokana na hali hiyo Wizara iliyona kuna haja ya kufanyia maboresho sera hiyo ili kutoa nafasi kwa watanzania kutoa maoni yao juu ya sera hiyo kwa ajili ya kuunda kesho yao na kuendana na wakati wa sasa na wakati ujao.

Kongamano hilo la kukusanya maoni lilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wanasiasa, viongozi wa dini, wazee wa Dar es salaam, wasomi, wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Dar es Salaam, makundi ya kijamii na vijana.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akiongea katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akiwasilisha mada kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Akifanya majumuisho ya kongamano hilo, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) alipata fursa ya kujibu baadhi ya hoja ambazo ziliibuliwa na washiriki wa Kongamano hilo.

Balozi Mbarouk amesema kuwa msimamo wa Tanzania toka enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa ni ule ule, haujabadilika, msimamo wa Tanzania kwa Palestina na Saharawi unajulikana vizuri na haujawahi badilika, siku zote Tanzania imekuwa ikitoa matamko yake.
Moja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mmoja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mmoja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam.

Alisema tangu yaanze mapigano kati ya Palestina na Israeli, Tanzania imeunga mkono matamko yote Saba ya Umoja wa Mataifa yaliyolenga kusitishwa kwa mapigano hayo na kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu.

“Hatujakataa azimio hata moja, maazimio yote yalilenga kusitishwa kwa mapigano hayo na kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu tuliyaunga mkono,” alisema Balozi Mbarouk.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news