NI MAFURIKO YA WATU:Usiku wa Maajabu chini ya Balozi wa Amani Duniani na Mtume Dkt.Peter Nyaga waweka rekodi mpya jijini Nairobi,wapokea uponyaji papo kwa hapo

NAIROBI-Kwa mara nyingine tena Balozi wa Amani Duniani na Mtume wa Urejesho kutoka RGC Miracle Centre Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam, Dkt.Peter Nyaga ameongoza maelfu ya watu kuupokea mwaka mpya 2024 jijini Nairobi nchini Kenya.
Kupitia mkesha huo mkubwa wa kuvuka mwaka uliofanyika Desemba 31,2023 kuanzia saa 1 jioni hadi asubuhi ndani ya Kawangare BP Stage, Uwanja wa Empowerment Centre uliopo karibu na Shell Petrol Station uliwaleta maelfu hayo ya watu huku wakipokea uponyaji wa papo kwa papo.

Dkt.Nyaga kwa jina la Yesu aliachilia uponyaji kwa mamia ya watu ambao waliponywa magonjwa sugu,kukombolewa na kufunguliwa katika vifungo vya shetani.

Licha ya watu kuwekwa huru dhidi ya vifungo vya shetani, pia Dkt.Nyaga aliwatamkia neno la baraka kwa mwaka 2024 watu wote huku akigawa fedha kwa ajili ya mitaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news