Wasudan waliopo Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhamishiwa Temeke

DAR ES SALAAM-Wanafunzi 20 wa udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST) cha Khartoum nchini Sudan wanatarajia kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH) kama moja ya hatua ya kuongeza ujuzi katika fani ya udaktari baada ya kukamilisha kipindi chao cha mafunzo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Uhamisho huo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) unatarajia kufanyika kuanzia Januari 2, 2024 kwa kuzingatia lengo la kuwawezesha kupanua ujuzi wao na kujifunza mazingira tofauti ya utunzaji wa afya.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt. Joseph Kimaro,amesema, "Tunafurahi kuwakaribisha wanafunzi hawa wa UMST katika timu yetu ya wataalamu wa afya, kwani tupo tayari kutoa ushirikiano kwa wanafunzi na kuhakikisha wanapata elimu bora na mafunzo sahihi yatakayowawezesha kuwa madaktari wenye ujuzi.”


Ameyasema hayo mara baada ya mazungumzo makini kati uongozi wa TRRH, na Profesa Mamoun Homeida kutoka Chuo cha Tiba, Sayansi na Teknolojia (UMST).
Wanafunzi hawa wana matarajio ya kujiunga na idara mbalimbali za hospitali hiyo, kama vile idara ya mifupa, watoto, Upasuaji, Upasuaji njia ya Mkojo, magonjwa ya ndani, na idara ya wanawake na uzazi. Kila idara inawakilisha fursa kwa wanafunzi hawa kuendeleza stadi zao na kujenga misingi imara ya ujuzi wa udaktari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news